Yanga imeendelea kutakata uwanja wa Taifa baada ya kuichapa Lipuli Fc mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mabingwa hao wa kihistoria walifunga mabao yao yote mawili kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Mapinduzi Balama (14') na Bernard Morrison (31')
Mabao yote yalitokana na krosi maridadi za Juma Abdul ambaye amerejea kwenye ubora wake
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao hayo mawili


Kipindi cha pili Yanga ilipunguza kasi na kuwapa nafasi Lipuli kufanya mashambulizi ambayo yaliwapatia bao la kufutia machozi liliilofungwa na David Mwassa kwa mpira wa adhabu
Ulikuwa ni mchezo ambao kama safu ya ushambuliaji ya Yanga ingekuwa makini, wangeweza kufunga mabao mengi
Ushindi huo umeifanya Yanga ichupe mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 34