Uwanja wa Uhuru unachukua takribani mashaniki 22,000 hivyo ni dhahiri idadi kubwa ya mashabiki watakosa nafasi ya kuushuhudia mtanange wa Yanga na Simba unaopigwa kwenye dimba la Uhuru keshokutwa Jumamosi.
Yanga ambayo ni wenyeji wa mchezo huo imepewa tiketi 12,000 kwa ajili ya mashabiki wake.
Jana Katibu Mkuu Charles Mkwassa alitahadharisha juu ya hofu ya kutokea vurugu uwanjani kutokana na ukweli kwamba mashabiki watakuwa na shauku ya kwenda dimbani.
Wakati Simba na Yanga zilipokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii katika dimba kuu la Taifa, mashabiki 44,000 waliingia kushuhudia mchezo huo.
Sasa uwanja wa Uhuru utachukua nusu ya mashabiki hao.
Pengine muda huu tayari tiketi za mchezo huo zitakuwa zimeisha hivyo ni vyema kwa wale watakaokosa tiketi wakafuata ushauri wa Mkwassa, wabakie nyumbani watazame mchezo kupitia TV zao.

ADVERTISE HERE