Kama ni kweli haya yanafanyika kwa maelekezo ni hatari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Feb 2020
Kama ni kweli haya yanafanyika kwa maelekezo ni hatari

Makala hii imeandikwa na Omary Katanga

Nimepitia "Comment" mbalimbali kwenye baadhi ya magroup ya whatsapp pamoja na mitandao mingine ya kijamii ikiwemo Facebook na Twitter, nikaona malalamiko na picha hiyo juu ikijadiliwa kwamba kumekuwa na mpango wa wazi kwa waamuzi kujifanya hawaoni matukio ya Offside wakati wa mchezo ukiendelea.

Malalamiko hayo yanaelekezwa kwa waamuzi kwamba wanatekeleza maelekezo (sijui yanatoka kwa nani) ya kuibeba klabu ya Simba katika mechi zake za hivi karibuni ili ipate ushindi na pointi nyingi ili itwae ubingwa kirahisi.

Hapa ni lazima tukubaliane mambo kadhaa;

(1). Kama ni kweli waamuzi wanapokea maelekezo hayo basi ni wazi kamati ya waamuzi imeshindwa kutimiza wajibu wake kwa kukiuka kwa makusudi kanuni na maudhui ya kuchezesha mechi

(2). Kama ni kweli yupo mtu/watu/ wanaotoa maelekezo kwa waamuzi kwa lengo la kuipendelea klabu fulani ili inufaike huku ikifahamika kwamba klabu nyingine zinatumia gharama na nguvu kubwa kusaka ushindi wa halali, basi ni wazi mtu/watu hao hawana nia njema ya maendeleo ya soka la tanzania

(3). Kama ni kweli wachezaji wa timu husika wanaufahamu mpango huu wa kubebwa (kama kweli upo) basi haitakuwa ajabu ikafika pahala wachezaji wakashindwa kutimiza wajibu wao kama inavyopaswa wakiamini kwamba iwe jua au mvua lazima wataondoka na pointi 3 baada ya mchezo

(4). Kama ni kweli mambo haya yapo, basi taifa lisubiri kushuhudia aibu kubwa inapofika muda wa uwakilishi kimataifa kwenye michuano ya vilabu barani afrika, kwa timu zetu kushindwa kuonesha ushindani halisi mbele ya wapinzani, maana kule hawatakwenda waamuzi wenye tabia ya kukinzana na sheria 17

(5). Kama ni kweli mambo hayo ya kubebana yapo kwenye soka letu, mamlaka ya soka TFF msikae kimya maana hii ni hatari inayoweza kuliweka taifa katika dimbwi la kushindwa kusimamia taratibu zilizoweka katika mchezo wa mpira wa miguu duniani,kwa kuzibinya jitihada halali za ushindani kwa klabu nyingine shiriki katika ligi

(6). Na kama mambo hayo ya kubebwa ni hisia tu za baadhi ya watu, dadhani ifike pahala mashabiki na wadau wote wa kandanda tuwe watulivu na kuziacha mamlaka kutimiza majukumu yao.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’