Kikosi cha Yanga leo saa moja usiku kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu
Baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo, mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wakisaka ushindi mwingine ili kuendelea kuweka hai matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu
Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema vijana wana ari na wamepania kuwapa furaha mashabiki, hivyo amewataka kujitokeza kwa wingi
Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-
"Sisi tuna timu bora, tunashinda michezo yetu kwa nguvu zetu hatutegemei kubebwa kama wanavyofanyiwa wengine. Mashabiki njooni kwa wingi mpate burudani kutoka kwa timu yenu," alisema Nugaz
ADVERTISE HERE