Huu hapa mkakati wa GSM kujenga Yanga Mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Feb 2020
Huu hapa mkakati wa GSM kujenga Yanga Mpya

Hii ni kutoka jikoni GSM;

Klabu ya Yanga ilitangaza kamati ambayo itasimamia na kuiongoza Yanga SC kuelekea mfumo wa kisasa, sisi kama GSM pamoja na kuwa na plan nyingi za kusaidia timu in terms of technical bench na wachezaji ambazo tayari tumezifanya kwa kiasi kikubwa, Juzi tumemleta pia mtaalamu mwingine kutoka south Afrika ambaye ataongezeka katika technical bench kuungana na Luc, Riedoh.

Hii yote ni kuifanya Yanga SC kuwa na nguvu.

Tunaendelea na tutaendelea kufanya vitu vingine ambavyo vipo nje ya mkataba , lengo ni kuendelea kuisaidia timu yetu ya Yanga SC

Tukizungumzia kambi ambayo timu inakaa na uwanja wa kufanyia mazoezi ni 100% GSM inasimamia

Tukaona haitoshi tu kuona timu ya Yanga inafanya vizuri uwanjani, tukaona tuwasaidie kuwapeleka katika mfumo ambao klabu itakuwa imara

Watu wengi wanaweza wakadhani GSM ina nia ya kuichukua Yanga, ama kuimiliki, hapana sisi lengo letu ni kuisaidia Yanga SC

Kamati iliyoundwa kusimamia mabadiliko ina watu weledi sana, lakini changamoto wengi hawawezi kujitolea 100% kusimamia mchakato huo kwa kuwa wamebanwa na majukumu mengine ikizingatiwa mabadiliko yanahitajika haraka sana

Kwa kuliona hilo ndio maana tukamleta mtaalam Antonio Pinto ambaye ana experience kubwa sana kutokea Benfica na atakuwa dedicated katika wajibu huo.

Amefanya mambo makubwa sana Benfica, ambapo wameuza wachezaji wenye thamani ya euro milioni 600 katika kipindi cha miaka 10, na wametwaa ubingwa mara 8 katika miaka 10

Huyu hajaja katika operation za Yanga, amekuja katika transformation project tunayoitarajia kuifanya kama klabu

Pinto anaondoka leo, amekuja kwa ajili ya makubaliano na majadiliano ambayo tayari tumeafikiana

Sisi GSM tumefanya miradi mingi sana ambayo haijawahi kufail na ipo very succesfull na huu mradi nakuhakikishia utakuwa very succesful.

Hatutaendana na zile njia ambazo watu wanazitumia, tutakwenda very profesional tutampa muda Pinto nakuhakikisha ana fikia malengo ya  hii project team itaenda bega kwa bega na kamati ya mabadiliko ya klabu ili kuhakikisha tunaendana na matakwa halisi ya nchi yetu

Pia tutafanya mabadiliko ya katiba ili kuendana na mabadiliko tunayoenda kufanya, hivi vitu vyote vitaenda parallel.

Muelekeo wetu ni kuisaidia Yanga SC isimame kwa miguu yake miwili

Infrastructure kuna trainning facility, sehemu ya kulala wachezaji na kuhakikisha viongozi wanakuwa na ofisi nzuri na zenye hadhi.

Muda mfupi tu nawahakikishia kila kitu kitabadilika Yanga SC na itakuwa ni klabu yenye mafanikio makubwa kuliko klabu yoyote ukanda wa Afrika mashariki na kati.

Eng Hersi Said (Mkurugenzi mwekezaji GSM)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’