Nchimbi ataja siri ya ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2020
Nchimbi ataja siri ya ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar

Mshambuliaji Ditram Nchimbi jana alitengeneza bao pekee la Yanga kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar

Nchimbi aliingia kwenye kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrick Sibomana na ilikuwa krosi yake kutoka winga ya kulia ambayo ilizaa bao hilo lililowekwa kimiani na David Molinga 'Falcao'

Nchimbi ambaye hivi karibuni alikwenda Misri kufanya majaribio klabu ya Smouha, amesema ushindi waliopata jana ulitokana na mafanikio ya mpango wa kocha Luc Eymael kwenye kipindi cha pili

"Mwalimu alinipa maelekezo kutokana na mechi ilivyokuwa ikiendelea kwa sababu aliyekuwa akicheza winga alikuwa akicheza taratibu. Alinitaka nitumie nafasi iliyokuwa ikiachwa na walinzi wa pembeni wa Mtibwa Sugar ambao walikuwa wakipanda sana. Mwisho wa siku mpango wake umefanikiwa na tumeweza kushinda"

Nchimbi amewataka mashabiki wa Yanga waendelee kuwaunga mkono kwani timu imeanza kucheza vizuri na wachezaji wameongeza kujiamini

Wana matumaini ya kufanya vizuri zaidi kwenye michezo inayofuata

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’