Walinzi Lamine Moro na Said Juma Makapu wameendelea kuibeba ya safu ya ulinzi wa Yanga ambapo jana walicheza pamoja katika mchezo wa tatu
Makapu aliyeingia kikosini kama mbadala wa mkongwe Kelvin Yondani, ameonyesha ubora katika michezo hiyo
Wawili hao wanaonekana kucheza kwa maelewano sana na kikubwa wameimarisha safu ya ulinzi ambayo kwenye michezo ya nyuma ilikuwa ikiruhusu mabao mara kwa mara
Tangu Moro na Makapu waanze kucheza pamoja, Yanga imeruhusu bao moja tu katika michezo mitatu iliyopita
Makapu amekomaa
Kocha Luc Eymael ameonesha kumuamini sana Makapu ambaye awali alikuwa akitumika zaidi kama kiungo mkabaji
Amekuwa akiimarika kwenye nafasi ya ulinzi kadiri siku zinavyosonga

Ni beki mtulivu asiye na mambo mengi, mara nyingi anakuwa na maamuzi sahihi pale anapokabiliana na washambuliaji wa timu pinzani
Kuimarika kwake kunaweza kumuweka matatani mkongwe Yondani ambaye siku za karibuni alimkera Eymael baada ya kukosa mazoezi kwa siku sita
Makapu pia anaonakana kuwa chaguo la kwanza mbele ya walinzi wengine Andrew Vicent na Ally Mtoni ambaye alireje akikosini jana kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kumaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu