Ivi bado kuna sababu ya kuijazia Yanga viporo?

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
29 Jan 2020
Ivi bado kuna sababu ya kuijazia Yanga viporo?

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa ambapo mchezo wa mapema ni kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Simba dhidi ya Namungo Fc

Lakini kinachoshangaza ni kuwa Yanga haitacheza mchezo wowote mpaka siku ya Jumapili watakapocheza na Mtibwa Sugar licha ya kuwa wana michezo miwili ya viporo

Kesho Mtibwa Sugar watacheza na Azam Fc na kisha watacheza na Yanga Jumapili!

Mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wamepumzika wiki nzima baada ya mchezo wao wa kombe la Azam dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulipigwa Jumapili iliyopita

Lakini pengine wangeweza kucheza angalau mchezo mmoja wa kiporo kabla ya Jumapili

Sidhani kama kuna sababu kuendelea kurundika michezo ya viporo kwa Yanga kwani baadae huenda ikasababisha ugumu wa ratiba na pengine watalazimika kucheza mfululizo

Pengine viongozi wa Yanga wanapaswa kuipigia kelele Bodi ya Ligi kuhakikishia wanawapangia mechi zao za viporo ili wazicheze sasa kujiepusha na changamoto ya ratiba ambayo huenda ikatokea baadae

Kwa siku za karibuni Yanga imekuwa kwenye kiwango kizuri, kucheza mechi wakati huu ingekuwa sahihi zaidi kuliko wanapokaa muda mrefu bila ya kucheza inaweza kuathiri 'form' yao

Kama viongozi wa Yanga hawataomba mechi hizo zipangiwe ratiba mapema, Bodi ya ligi itatafuta wakati wanaoona inafaa kuwapangia kucheza

Kwa sasa hakuna sababu kwa timu kutofautiana hadi michezo mitatu wakati hakuna timu inayoshiriki michuano ya Kimataifa

Kwani wakati Yanga wao wanasubiri kucheza Jumapili, wenzao Simba watakuwa wameshacheza mechi mbili, leo na Jumamosi hivyo kutakuwa na tofauti ya michezo mitatu kati yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’