Nahodha wa zamani wa Yanga Kelvin Yondani huenda akarejeshwa kikosini kwenye mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa siku ya Jumapili Februari 02 kwenye uwanja wa Uhuru
Yondani alikosa michezo mitatu iliyopita, akikosa mazoezi kwa siku sita kutokana na sababu alizoeleza kuwa mgonjwa
Kitasa huyo wa timu ya Taifa alirejea kikosini siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons hata hivyo Eymael hakumtumia kwenye mchezo huo
Leo anatarajiwa kuendelea na mazoezi ya kikosi cha Yanga baada ya mapumziko ya siku mbili
Juzi Eymael alieleza kutofurahishwa na mazingira ya kukosekana kwake kikosini
Eymael aliwatahadharisha wachezaji kuwa ni lazima wazingatie nidhamu kama wanataka kupata nafasi kwenye kikosi chake
Alisisitiza kuwa hakuna mchezaji mtovu wa nidhamu ambaye atapata nafasi ya kucheza na kuwa hakuna mchezaji mkubwa kuliko Yanga