Miongoni mwa maboresho ya Katiba ambayo yatafanywa na Wanachama wa Yanga kwenye Mkutano Mkuu wa dharura ambao utafanyika Februari 16 2020, ni pamoja na kutambuliwa rasmi usajili wa Wanachama kwa mfumo wa kidigitali
Huo ndio utakuwa utaratibu rasmi wa usajili wa Wanachama wa Yanga ambapo baada ya kusajiliwa Mwanachama atapewa kadi ya ki-elektroniki
Faida zitakazopatikana kutokana na mfumo huo;
i). Klabu itakusanya mapato kutoka kwa Wanachama wake kwa njia rahisi, salama na bora
ii). Klabu itaweza kutambua na kuhifadhi takwimu za Wanachama wake kwa mfumo wa kidigitali
iii). Mwanachama atanufaika na kadi ya uanachama wake kwa kupata stahiki mbalimbali mfano Bima, mikopo midogo midogo, punguzo la bidhaa za Yanga n.k
iv). Uwepo wa idadi ya wanachama waliojiandikisha utainufaisha Yanga kupata udhamini na uhisani
v). Pia itarahisisha uhakiki wa Mwanachama pale atakapotaka kununua hisa kwenye mfumo mpya wa uwekezaji