Mkufunzi wa Yanga Luc Eymael amemzuia kiungo mshambuliaji Bernard Morrison kuacha au kuchagua muda sahihi wa kufanya mbwebwe wakati anapokuwa dimbani
Eymael amesema hafurahishwi na matukio ya kufedhehesha mpinzani kwani kwenye mpira mpinzani anatakiwa kuheshimiwa
"Mashabiki wanapenda zile mbwembwe za Morrison, upande wangu sipendi na nilimwambia asifanye vile au kama atataka kufanya basi afanye dakika za mwisho timu ikiwa tayari imepata matokeo," amesema
"Huwa sipendi mzaha ndio maana hata ulaya hakuna mambo hayo. Salah anafanya hayo? Mane Je?Messi hafanyi pia. .Japo najua Afrika mnapenda, binafsi sipendi kumfedhehesha mpinzani"
"Katika mpira mpinzani anapaswa kuheshimiwa, kwangu sio sawa"
ADVERTISE HERE