Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons jana, kikosi cha Yanga kitashuka tena dimbani Jumapili February 02 kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Huu utakuwa mchezo wa kisasi kwa Yanga ambayo iliondoshwa na Mtibwa Sugar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1
Mabingwa hao wa kihistoria, wanatarajiwa kuendeleza bando la burudani kwa mashabiki wake ambao kwa sasa wamerejesha hamasa kwa timu yao
Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea tena dimba la Uhuru siku tatu baadae, Februari 05 kuikaribisha Lipuli Fc
Ni michezo ambayo Yanga inahitaji kuondoka na alama zote sita kabla ya kuanza ratiba ya michezo ya mikoani
ADVERTISE HERE