Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Singida United dhidi ya Yanga utapigwa katika uwanja wa Namfua Novemba 04 baada ya ukarabati wa uwanja huo kukamilika.
Yanga itakuwa timu ya kwanza kucheza katika uwanja huo uliofanywa kuwa wa kisasa.
Klabu ya Singida United imethibitisha kuwa itaanza kuutumia Uwanja wake wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Novemba 4, mwaka huu.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amebainisha kwamba uwanja huo uko tayari kwa matumizi baada ya ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch)
Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.
Tayari uwanja wa Jamhuri Dodoma (pichani Juu) umefungwa kwa ajili ya ukarabati mkubwa.

ADVERTISE HERE