Winga wa zamani wa Yanga Saimon Msuva ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, ametwaa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa timu hiyo
Msuva alitangazwa kushinda tuzo hiyo kwenye hafla iliyofanyika jana nchini Morocco
Tuzo hiyo ni heshima kubwa kwake pamoja na Taifa lake la Tanzania
Tangu atue Difaa miaka mitatu iliyopita akitokea klabu ya Yanga, Msuva amekuwa mchezaji wa kutegemewa

ADVERTISE HERE