Hili la Wawa haliwezi kupita hivihivi

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
23 Jan 2020
Hili la Wawa haliwezi kupita hivihivi

Jana Kamati ya Saa 72 ilitoa adhabu mbalimbali kwa timu zinazoshiriki ligi kuu kulingana na makosa mbalimbali yaloyofanyika kwenye ligi tangu kuanza kwa mwaka huu

Wakati Yanga ikionekana kinara wa kuadhibiwa, kuna matukio ya dhahiri ambayo yalijitokeza lakini wengi wanashangaa hatua hazikuchukuliwa

Zaidi ni tukio la beki wa Simba Paschal Wawa kumkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Januari 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa

Pamoja na kuwa mwamuzi hakuliona tukio hilo, kamera za Azam Tv zililinasa na hata Mwenyekiti wa Bodi ya ligi aliahidi kuwa hatua zitachukuliwa

Lakini katika matukio yaliyotolewa adhabu jana tukio la Wawa halikuwa miongoni

Wakati mwingine matukio kama haya ndio yanayowapa sababu watu kuamini kuwa TFF na Bodi ya Ligi zinafanya kazi kwa kuipendelea klabu ya Simba

Kwani wakati mashabiki wa Yanga wakilalamikia tukio la Wawa, mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere alimpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa uhuru mwaka jana

Lakini pamoja na tukio hilo kupigiwa kelele hakuna hatua zozote zilizochukuliwa

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Steven Mguto jana alisema baadhi ya matukio bado yanachunguzwa

Wadau hawatachoka kusubiri kuona kama hatua zinachukuliwa ili kuondoa hii dhana ya kuwa kuna upendeleo unafanywa kwa baadhi ya timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’