FT : Singida United 1-3 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jan 2020
FT : Singida United 1-3 Yanga

Yanga leo imetakata uwanja wa LITI (zamani Namfua) mkoani Singida baada ya kuichapa Singida United mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu

Vijana wa kocha Luc Eymael waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na shauku ya kuondoka na alama zote tatu na hilo wamelitimiza kibabe kabisa

David Molinga alianza kuifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 12 akimalizia pasi murua ya Mapinduzi Balama

Mabingwa hao wa kihistoria walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo moja

Bao la pili liliwekwa kimiani kwenye dakika ya 58 na Haruna Niyonzima aliyeachia shuti kali baada ya kukutana na krosi ya chini kutoka kwa Bernard Morrison aliyekuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Singida United

Mu Ivory Coast Yikpe Gnamien aliyeingia kuchukua nafasi ya David Molinga, aliiongezea Yanga bao la tatu kwenye dakika ya 78 wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Singida United lilifungwa na Six Mwasekaga

Kikosi cha Yanga leo kilitandaza kandanda safi la kushambulia kwa kasi huku wakikaba kwa nguvu pale walipopoteza mpira

Kwa muda mrefu mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata alikuwa hapati kashikashi kutoka kwa washambuliaji wa Singida United kutokana na uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga

Singida United walitengeneza mashambulizi wakati mchezo huo ukielekea ukingoni

Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha Luc Eymael ambaye taratibu matunda ya kazi yake yameanza kuonekana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’