Mshambuliaji hatari wa Yanga Donald Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga.
Ngoma aliyewasili jana kutokea kwao nchini Zimbabwe amemalizana na uongozi wa Yanga mapema leo na kusaini mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga.
Jana kuliripotiwa taarifa na mtandao mmoja wa Afrika Kusini kuwa mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Polokwane City inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Ngoma amekiri kufanya mazungumzo na klabu hiyo lakini amekana kusaini mkataba na kudai taarifa zilizoripotiwa na mtandao huo ni za uongo.
Mchezaji huyo pia alikuwa akiwaniwa na Simba lakini pengine taarifa za kusaini Polokwane City ziliwapoteza viongozi wa Simba waliokuwa wamejiandaa kumpokea uwanja wa ndege.
Ngoma alitua JNIA jana jioni na akapokelewa na maafisa wa ulinzi wa klabu ya Yanga.

ADVERTISE HERE