Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema baada ya benchi la ufundi kufanyia kazi changamoto zilizowafanya wakose matokeo kwenye michezo iliyopita, leo wamepania kuibuka na ushindi mkoani Singida
Jioni ya leo Yanga itachuana na Singida United katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Namfua
Mabingwa hao wa kihistoria wanasaka alama tatu baada ya kuzikosa kwa takruibani dakika 270
Abdul amewataka mashabiki kutokata tamaa kwani timu yao sasa iko tayari kuwapa furaha
"Napenda kuwaambia mashabiki wetu wasikate tamaa, kila kitu kimerekebishwa kuelekea mechi ya leo jioni," amesema
"Yanga itatengamaa na tutapambana kupata ushindi , bado kocha mpya alikuwa anakijenga kikosi sasa tupo tayari kwa mapambano"
ADVERTISE HERE