Kwa sasa ukizungumzia wachezaji wanaofanya vizuri nchini Tanzania, huwezi kukosa kutaja jina la kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama
Balama aliyetua Yanga mwezi Julai 2019 akitokea klabu ya Aliiance Fc, ameweza kuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Pamoja na kufundishwa na makocha watatu tofauti katika kipindi cha miezi mitano, Balama ameweza kuwa na nafasi katika vikosi vya kwanza vya makocha wote kuanzia wakati wa Mwinyi Zahera, Charles Mkwasa na sasa Luc Eymael
Kuna wakati Zahera alitamba kuwa na kinda huyo kwenye kikosi chake, mwenyewe alimtumia katika nafasi tofauti tofauti na aliweza kufanya vizuri
Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Balama anaweza kufikia mafanikio ya juu kama ataheshimu kipaji chake na kuongeza juhudi na kujiwekea malengo ya kufika mbali

Kutokana na mafanikio ya wachezaji kama Simon Msuva na zaidi Mbwana Samatta aliyesajiliwa na Aston Villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, Mawakala wengi kutoka barani Ulaya wameanza kutupia jicho nchini Tanzania kusaka vipaji
Kwani katika kipindi cha miaka miwili tumewashuhudia nyota wengi wa Kitanzania wakipata nafasi ya kuitwa kufanya majaribio Ulaya na wengine kusajiliwa huko au hapahapa barani Afrika
Ni nafasi kwa Balama na nyota wengine wa Kitanzania kujiwekea malengo ya kufika mbali na kujituma kuhakikisha wanatimiza malengo hayo