Mjadala : Mkwasa aondoke au abaki?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jan 2020
Mjadala : Mkwasa aondoke au abaki?

Mwezi huu Yanga imemleta kocha mpya Luc Eymael kuwa mrithi wa Mwinyi Zahera aliyetimuliwa mwezi Novemba 2019

Lakini kabla ya ujio wa kocha mpya, Yanga ilikuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa

Kumekuwa na mjadala juu ya nini kinaisibu Yanga sasa kwani tangu Eymael awasili timu imefungwa mechi zote

Wapo wanaodhani kuna jambo haliko sawa kwenye benchi la ufundi

Baadhi wametoa maoni kuwa ni vyema uongozi wa Yanga ukamuondoa Mkwasa kwenye benchi la ufundi ili kuwaacha makocha wapya wawe huru kutimiza majukumu yao

Kocha Kenny Mwaisabula ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, amesema Mkwasa tayari amemaliza majukumu yake hivyo hapaswi kuendelea kuwa kwenye benchi la ufundi

Lakini pia wapo wanaoamini Mkwasa anastahili kuendelea kuwepo ili kuwasaidia makocha wapya kwani bado hawawafahamu wachezaji

Je mdau ni yepi maoni yako, Mkwasa aondolewe kwenye benchi la ufundi au abakishwe?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’