Mchezo dhidi ya Singida United ambao utapigwa keshokutwa Jumatano uwanja wa Namfua una umuhimu wa kipekee kwa Yanga
Ukweli ni kwamba Yanga inapita katika kipindi kigumu kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha
Kupoteza michezo dhidi ya Kagera Sugar na Azam Fc kumeongeza presha kwa mabingwa hao wa kihistoria
Aidha mashabiki nao wametakiwa kuwa wamoja kipindi hiki ili kuhakikisha timu haigawanyiki
Kocha Luc Eymael atahitaji kuhakikisha Yanga inaondoka na alama zote tatu mkoani Singida katika mchezo ambao hautakuwa mwepesi
Kwani mwendelezo wa matokeo mabaya utamuweka katika presha kubwa
ADVERTISE HERE