Bado tunatengeneza timu - Abdul

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jan 2020
Bado tunatengeneza timu - Abdul

Nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema pamoja na kupoteza michezo miwili mfululizo, watarejesha makali yao

Akizungumza baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Azam Fc, Abdul amesema matokeo hayo hawakuyatarajia kwani walikuwa wamejipanga kuibuka na ushindi

"Kama wachezaji tumepambana tangu dakika ya kwanza lakini bahati haikuwa kwetu," amesema

"Tumetengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia wenzetu wamepata nafasi moja, wameitumia"

Aidha Abdul amewataka mashabiki wa Yanga kutokata tamaa na timu yao kwani kila kitu kitakuwa sawa

"Tunawaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono. Lazima wafahamu kuna mabadiliko yametokea kwenye timu yetu. Mwanzo tulikuwa na Zahera, alipoondoka tukawa na Mkwasa kwa muda na sasa tunae kocha mwingine"

"Kila kocha ana mbinu zake ambazo tunahitaji muda kuweza kuzishika. Lakini pia kuna wachezaji wameondoka na wengine wapya kusajiliwa, nao wanahitaji muda kuzoea"

"Mwalimu bado anatengeneza timu, mashabiki wawe na subira, tutakuwa sawa kama zamani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’