Mchezo dhidi ya Kagera Sugar Mohammed Issa 'Banka' alipewa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano
Kutolewa kwake kulichangia kwa kiasi kikubwa Yanga kupoteza mchezo kwa kuchapwa mabao 3-0
Leo katika mchezo dhidi ya Azam Fc beki Ally Mtoni alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumkanyaga Nicholas Wadada
Sonso hakuwa na siku nzuri kwani katika kipindi cha kwanza alijifunga bao lililoipa ushindi Azam Fc
Beki huyo aliyetua Yanga kutoka Lipuli Fc anatarajiwa kukosa michezo mitatu
Pengine benchi la ufundi linapaswa kuzungumza na wachezaji ili wajiepushe na matukio ambayo yanapelekea wapewe kadi zisizo za lazima
Kwani tukio la kadi ya Mtoni leo hakupaswa kulifanya pamoja na kuwa ni yeye aliyeanza kufanyiwa madhambi