Kikosi cha Yanga kimebaki Shinyanga kwa mapumziko ya siku moja baada ya ushindi wa jana wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Stand United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema timu itaondoka Shinyanga kesho Jumanne asubuhi kwa basi kurejea Dar es Salaam na inaweza kuingia kambini kuanzia Jumatano kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Simba.
Yanga watamenyana na mahasimu wao wa jadi, Simba katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba Yanga ingeweka kambi mkoani Morogoro lakini kutokana na mabadiliko hayo inatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam Jumanne usiku hivyo uwezekano wa kwenda Morogoro ni mdogo kwa kuwa zitakuwa zimebaki siku mbili tu za maandalizi.
Yanga inaweza kuweka kambi Kigamboni, moja ya maeneo ambayo imekuwa ikiyatumia kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba.
Simba tayari imeelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE