Mtibwa Sugar wametawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2020 baada ya kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar
Mtibwa Sugar iliyokuwa bora dhidi ya wapinzani wao Simba, ilijipatia bao la ushindi kwenye dakika ya 38 likiwekwa kimiani na Awadh Salum
Vijana hao wa Zuberi Katwila wametwaa ubingwa wa pili wa michuano hiyo tangu kuanzishwa kwake huku mwaka huu wakiweka rekodi ya kuzifunga Yanga na Simba
Lakini ushindi wao dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali ulikuwa wa mikwaju ya penati
Mtibwa Sugar imeshinda taji pamoja na kitita cha Tsh Milioni 15
ADVERTISE HERE