Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael ameeleza kuridhishwa na uwezo wa wachezaji wa kikosi chake hivyo kumpa matumaini wanaweza kufanikisha malengo waliyowekewa
Eymael ambaye leo alianza majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria, amesema kikosi chake kina wachezaji wengi wazuri, kazi yake kubwa sasa ni kuwaunganisha ili kutengeneza timu ya ushindani
Amesema timu yake haihitaji mabadiliko makubwa sana ya kiufundi, atakachokifanya ni kuongeza mbinu kwa wachezaji
"Sioni kama nahitaji kufanya mabadiliko makubwa sana, nimeona mazuri mengi kutoka kwa wachezaji, nadhani kazi yangu haitakuwa kubwa sana hapa," alisema Eymael baada ya kumaliza program ya mazoezi ya asubuhi leo



Kibarua cha kwanza cha kocha huyo Mbelgiji ni dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumatano, Januari 15 katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Mchezo wake wa pili utakuwa dhidi ya Azam Fc Januari 18 na baadae kuiongoza Yanga kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons Januari 25
Eymael amepewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuinoa Yanga pamoja na msaidizi wake Riedoh Berdien ambaye pamoja na kuwa kocha wa viungo, atakuwa kocha msaidizi wa pili