Kocha mpya wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael tayari ameanza majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Mchezo wake wa kwanza utakuwa siku ya Jumatano, Januari 15 dhidi ya Kagera Sugar na kisha kurejea tena dimbani siku tatu baadae kuikabili Azam Fc
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa Eymael amepewa mkataba wa miezi sita lakini mkataba huo utahuishwa mwishoni mwa msimu kama atafanikisha malengo aliyopewa
Jukumu kubwa alilopewa na GSM ni kuhakikisha anaiwezesha Yanga kushiriki michuano ya CAF msimu ujao kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu au kushinda kombe la Shirikisho
Lakini kipaumbele ni kushinda taji la ligi kuu
Eymael anaichukua Yanga mikononi mwa kocha Charles Mkwasa ambaye katika kipindi chake timu haikupoteza mchezo
Yanga inashika nafasi ya sita ikiwa na alama 25 baada ya kushuka dimbani mara 12
Mechi za wiki ijayo dhidi ya Kagera Sugar na Azam Fc ni kipimo chake cha kwanza