Mshambuliaji wa Yanga David Molinga huenda asirejee nchini kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria baada ya mkataba wake kusitishwa, imefahamika
Molinga alipewa ruhusu kwenda kwao Ufaransa kushughulikia matatizo binafsi lakini mshambuliaji huyo mkataba wake wa mkopo umesitishwa na Yanga, nafasi yake inachukuliwa na Owe Bonyanga aliyetokea klabu ya TP Mazembe
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa Molinga ameponzwa na kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya katika mchezo dhidi ya Biashara united
Molinga alifanyiwa mabadiliko na kocha Charles Mkwasa halafu akaelekea moja kwa moja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, akabadili mavazi yake kisha kuchukua usafiri wa bodaboda na kutokomea kusikojulikana
Kitendo hicho kilitafsiriwa kama dharau kwa kocha Mkwasa, benchi la ufundi na uongozi wa Yanga kwa ujumla
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wataongeza wachezaji wawili wa kigeni, Owe Bonganya ni mmoja wao na wa pili anaweza kuwa kiungo James Kotei ambaye huenda akatua nchini kesho