Ajib amtia presha Omog

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
23 Oct 2017
Ajib amtia presha Omog
Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog amekiri mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Jumamosi ijayo utakuwa mgumu kutokana na ubora ulioonyeshwa na kikosi cha Yanga siku za hivi karibuni.

Kocha huyo aliyekalia kuti kavu amekiri kuwa anahitaji kuwaandaa walinzi wake ipasavyo kuweza kumlinda mshambuliaji aliye kwenye kiwango bora sasa, Ibrahim Ajib.

Ajib amekuwa moto wa kuotea mbali ndani ya kikosi cha Yanga ambapo jana ameiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United, wenyewe akifunga mabao mawili.

Obrey Chirwa ni mchezaji mwingine ambaye anahofiwa na Omog.

“Nimewaangalia Yanga, wana timu nzuri Ajibu na Chirwa ni miongoni mwa wachezaji hatari kwa sasa katika kikosi hicho na katika mechi yetu nitahakikisha hawapati nafasi ya kupewa pasi za hatari ambazo zitakuwa na madhara langoni kwetu,” amenukuliwa Omog na moja ya magazeti ya Michezo.

“Ajibu nilikuwa nae katika kikosi changu msimu uliopita na ana uwezo wa kukaa na mpira akapiga pasi ya mwisho ambayo itakuwa na madhara kwetu, lakini anaweza wa kufunga muda wowote kama atapata nafasi.

“Chirwa ana uwezo wa kukaa na mpira na ana uwezo wa kukimbia huku akiwa na mpira mguuni na anaweza kufunga pia, nimeliona hilo na nitakaa na wachezaji wangu ili kuhakikisha hawapati nafasi kama hizo.”

Yanga na Simba zinakutana kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa nane Jumamosi ijayo, Oktoba 22 Yanga ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →