Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi, kikosi cha Yanga kinarejea jijini Dar es salaam leo kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, mchezo huo utapigwa Januari 15 2020 kwenye uwanja wa Taifa
Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael atakuwa na takribani siku nne za kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo huo ambao utapigwa saa moja jioni
Pengine kuondoshwa mapema katika michuano ya kombe la Mapinduzi ni ahueni kwa Yanga kwani kama ingetinga fainali, ingecheza Januari 13 kisha kushuka dimbani siku mbili baadae kuikabili Kagera Sugar
ADVERTISE HERE