Kocha Mkuu wa Yanga Luc Aymael amesema ujio wake ni maalum kurejesha makali ya mabingwa hao wa kihistoria
Aymael tayari ametua visiwani Zanzibar kukishuhudia kikosi chake kikipepetana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi
Mbelgiji huyo amesema ni furaha kwake kujiunga na Yanga, moja ya vilabu vyenye historia kubwa barani Afrika
"Nafurahi kuwa hapa na kuwa sehemu ya kikosi cha timu kubwa barani Afrika , Yanga,"Β Aymael aliwaambia Wanahabari
"Nipo hapa kwa maana kubwa moja tu, kuirudisha Yanga katika nyakati zile za ushindi na kuwapa furaha mashabiki wake
"Nawaahidi wapenzi na wanachama wa klabu hii tutafanya kazi kwa bidii kuiimarisha timu yetu, Leo ntakuwa uwanjani kuwatizama vijana wangu ili nipate taswira wapi pa kuanzia"
Aymael amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Anatarajiwa kusaidiana na Charles Mkwasa ambaye atabakishwa kuwa kocha msaidizi