Mkufunzi mpya wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika kwani amefundisha timu nyingi barani Afrika zikiwemo Rayon Sports ya Rwanda, AS Vita Club ya DRC, El Merreikh ya Sudan na AFC Leopards ya Kenya
Miongoni mwa mafanikio aliyopata katika vilabu mbalimbali barani Afrika
1. Ubingwa wa Ligi kuu ya DR Congo, akiwa na AS Vita Club (2010)
2. Ubingwa wa Ligi kuu ya Gabon na Missile FC (2012)
3. Alishinda Super cup ya DRC, akiwa na AS Vita Club (2011)
4. Alishinda National Cup ya Kenya, akiifundisha AFC Leopards (2013)
5. Alishinda pia kombe la Nedbank nchini Afrika Kusini, akiinoa Free State Stars (2018)
Luc ana UEFA Pro License, ambayo ni level ya juu kabisa ya leseni za ukocha barani ulaya
Alipata leseni hii mwaka 2007 huku leseni ya UEFA (UEFA license A) aliipata mwaka 2002.
Pia ana leseni ya CAF daraja A ambayo aliipata mwaka 2015 nchini Tunisia.
Amewahi kufanya kazi na wachezaji wengi wa Ubeligiji wa sasa na zamani kama Eden Hazard, Alex Witsel, Logan Bailly, Christian Benteke ambao aliwasaidia katika ukuaji wao katika mpira wa miguu