Sio tetesi tena kwani uongozi wa klabu ya Yanga umemtambulisha Mbelgiji Luc Eymael kuwa kocha wake mkuu akichukua nafasi ya Mwinyi Zahera
Kocha huyo anatarajiwa kuwasili nchini leo kukamilisha taratibu nyingine kabla ya kutambulishwa rasmi
Ni GSM wadhamini wa klabu ya Yanga ambao wamefanikisha ujio wake
Huenda Eymael atasaidiwa na Charles Boniface Mkwasa 'Master' nafasi ya kocha msaidizi
Mkwasa aliyeibuka kuwa kocha bora wa VPL kwa mwezi Disemba 2019, ameiongoza Yanga kwa mafanikio tangu alipokabidhiwa mwezi Novemba mwaka jana
Chini yake Yanga haikupoteza mchezo wowote wa kimashindano
ADVERTISE HERE