Uongozi wa Yanga uko kwenye hatua za mwisho kumalizana na Luc Eymael kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera aliyetimuliwa mwezi Novemba 2019
Eymael raia wa Ubelgiji, alikuwa akiinoa Black Leopards ya Afrika Kusini
Anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kumalizana na Yanga ujio wake ukisimamiwa na GSM
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60, ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika
Baadhi ya timu ambazo amewahi kuzifundisha ni pamoja na AS Vita, Rayon Sports, AL Nasr, Polokwane City, Free State Stars na Black Leopards ikiwa klabu yake ya sasa
ADVERTISE HERE