Niyonzima autaka ubingwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2020
Niyonzima autaka ubingwa Yanga

Akiwa bado hana hata wiki mbili tangu arejee klabu ya Yanga, kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima amesema wamedhamiria kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Niyonzima alijiunga na Yanga Alhamisi iliyopita na siku ya Jumamosi akacheza mechi dhidi ya Simba akiwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2

Niyonzima amesema amekuja nchini kuisaidia Yanga kurejesha ubingwa wa ligi kuu walioupoteza kwa watani zao Simba kwa misimu miwili sasa

Pamoja na kukiri kuwa wanahitaji kufanya kazi ya ziada kuwapoka ubingwa Simba, lakini wamejipanga

"Simba wana timu nzuri pengine kuliko hata nilipokuwa nikicheza msimu uliopita. Walitupa changamoto kubwa tulipocheza nao wiki iliyopita, Lakini juhudi za wachezaji pamoja na uzoefu vilituwezesha kusawazisha mabao mwili waliyotufunga," amesema

"Tunafahamu tutapata upinzani mkali kutoka kwao na timu nyingine lakini tutapambana ili kuhakikisha tunafanikisha dhamira yetu"

Niyonzima ni mmoja wa wachezaji wapya watano waliosajiliwa na Yanga dirisha dogo ili kukiongezea nguvu kikosi hicho

Wengine ni Ditram Nchimbi, Tariq Seif, Yikpe Gnamien na Adeyum Saleh

Yanga pia imemleta mshambuliaji Owe Bonyanga kutoka klabu ya TP Mazembe ambaye pia huenda akasajiliwa kuchukua nafasi ya David Molinga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’