Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amesajiliwa na timu ya Gor Mahia, mabingwa wa ligi kuu ya Kenya
Gor Mahia imemsajili Balinya baada ya kujiridhisha na uwezo wake
Balinya aliyekuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda, awali alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili
Hata hivyo alidumu Yanga kwa miezi sita tu, kabla ya makubaliano ya kuvunja mkataba baina yake na Yanga kufikiwa
Nyota huyo ni kama amepishana na Yikpe Gnamien aliyesajiliwa na Yanga akitokea Gor Mahia
ADVERTISE HERE