Nyota wa zamani wa Yanga Saimon Msuva amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu ya Benfica ya Ureno.
Meneja wa nyota huyo Jonas Tiboroha amethibitisha kuwa licha ya kusainiwa na Benfica atapelekwa kwa mkopo Panathinaikos ya Ugiriki kwa miezi 6 hivyo Msuva atajiunga rasmi na Benfica mwezi Julai
Msuva alitua Difaa El Jadid akitokea Yanga aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa
Msuva atakuwa mchezaji wa pili kutoka Tanzania kusajiliwa na timu kubwa barani Ulaya akiungana na Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk
Habari njema zaidi ni kuwa huenda Yanga ikapata sehemu ya fungu la mauzo ya nyota huyo kulingana na makubaliano waliyoingia na Difaa wakati wa mauzo yake
ADVERTISE HERE