Kikosi cha Yanga leo saa mbili na robo usiku kitashuka kwenye uwanja wa Amaan visiwai Zanzibar kuikabili Jamhuri kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Mapinduzi
Yanga iko visiwani Zanzibar tangu juzi usiku ikijiwinda na mchezo huo ambao ushindi utawapeleka moja kwa moja nusu fainali
Tayari Mtibwa Sugar na Azam Fc ambazo zilicheza jana, zimetinga nusu fainali baada ya kushinda michezo yao
Mapema Simba itacheza na Zimamoto kisha kufuata mchezo wa Yanga baadae
Kama Yanga itaibuka na ushindi itacheza na Mtibwa Sugar hatua ya nusu fainali wakati iwapo Simba itaifunga Zimamoto itacheza na Azam Fc nusu fainali
Yanga imetinga visiwani Zanzibar ikiwa na kikosi chake kamili akiwemo mshambuliaji mpya Owe Bonganya
ADVERTISE HERE