Wakati mashabiki wa Simba wakimlaumu mlinda lango Aishi Manula kufuatia matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Yanga, Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amemwagia sifa kiungo Mapinduzi Balama ambaye alifunga bao la kwanza
Balama alimtungua Manula kwa shuti kali akiwa nje ya 18 bao ambalo limepelekea mashabiki wa Simba kumtia matatani mlinda lango wao
Bumbuli anaamini 'bunduki' ile ilipigwa kiufundi zaidi na mlinda lango yeyote angefungwa
Amemtaka kiungo huyo aendeleze moto huohuo wa kuwanyoosha
"Acha leo waendelee kumlaumu kipa kana kwamba wewe hukufanya jambo, nakuhakikishia siku moja hawahawa wataweka mfano wa bao lako. Endeleza mapambano," amesema
Mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji ni miongoni mwa waliolisifia bao hilo lakini pia mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi alisema Balama anastahili kupewa sifa kwa kufunga bao lile badala ya kumlaumu Manula