Tukio lililofanywa na beki wa Simba Paschal Wawa kumkanyaga kwa makusudi mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi, limeibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambapo wadau wametaka TFF imchukulie hatua beki huyo
Tukio hilo ambalo lilinaswa na kamera za Azam Tv, limemuonyesha dhahiri Wawa akimkanyaga Nchimbi baada ya kumsukuma na kumuangusha nje ya uwanja
Wadau wanasubiri kuona hatua gani Kamati ya saa 72 itachukua baada ya tukio hilo
Msimu uliopita Kelvin Yondani alifungiwa mechi tatu baada ya kumfanyia tukio lisilo la kiungwana Asante Kwasi
Licha ya mwamuzi kutoliona wakati wa mchezo, Kamati ya saa 72 ilitumia picha za video kutoa adhabu hiyo
ADVERTISE HERE