Mshambuliaji David Molinga ameingia mtatani kwa uongozi wa Yanga akituhumiwa kwa matukio ya utovu wa nidhamu
Inaelezwa tukio alilolifanya kwenye mchezo dhidi ya Biashara United kwa kuondoka uwanjani baada ya kufanyiwa mabadiliko, limewakera mabosi wa Yanga
Lakini pia hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Molinga kufanya utovu wa nidhamu baada ya kufanyiwa mabadiliko
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa hakumjumuisha Molinga kwenye kikosi chake kilichotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba jana
Molinga hakuwekwa hata miongoni mwa wachezaji wa akiba
Molinga ambaye alitua Yanga kwa mkopo huenda akarejeshwa Congo
Tayari Yanga imeanza mchakato wa kusaka mshambuliaji mwingine
ADVERTISE HERE