Leo Yanga inashuka kwenye dimba la Kambarage mkoani Shinyanga kuchuana na Stand United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa saba.
Wakati akiwa tayari anawakosa Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Donald Ngoma, kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina huenda akafanya mabadiliko zaidi kwenye kikosi chake kitakachoshuka dimbani leo.
Sababu ya mabadiliko hayo inaweza kutokana na mipango yake kuelekea mchezo wa wiki ijayo dhidi ya Simba.
Ni hivi; wachezaji Kelvin Yondani, Juma Abdul na Raphael Daudi kila mmoja ana kadi mbili za njano.
Iwapo atawatumia katika mchezo wa leo na yeyote miongoni mwao akapata kadi ya njano, atakosa mchezo dhidi ya Simba.
Hofu hiyo inaweza kupelekea Lwandamina kulazimika kuwatumia kwa tahadhari katika mchezo wa leo.
Na kwa hali ilivyo na hasa ukizingatia wachezaji hao ni muhimu katika kikosi cha kwanza cha Yanga, wako hatarini zaidi kupata kadi.

ADVERTISE HERE