Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Simba licha ya kuwakosa Lamine Moro na Tariq Seif
Moro anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano (mbili ligi na moja FA) wakati Tariq alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Biashara United
Hata hivyo Mkwasa amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa kukosekana kwa wachezaji hao hakuwezi kuiathiri timu kwani wapo wachezaji wa kuchukua nafasi zao
Huenda atawatumia Kelvin Yondani na Ally Mtoni au Andrew Vicent kama walinzi wa kati huku safu ya ushambuliaji akiwategemea David Molinga, Ditram Nchimbi na Yikpe Gnamien
ADVERTISE HERE