Mashabiki wa Yanga wameaswa kuchangamkia tiketi mapema ili kuhakikisha wanaingia kwa wingi uwanja wa Taifa kesho kuwapa sapoti wachezaji
Pamoja na maandalizi mazuri, hamasa ya mashabiki uwanjani ina umuhimu mkubwa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema ni vyema mashabiki wakate tiketi mapema ili kuepuka usumbufu ambao utaweza kujitokeza siku ya mchezo
Aidha wadhamini wa Yanga, kampuni ya GSM wametoa ofa ya tiketi kwa kila shabiki anayenunua jezi orijino 'brand' chapa GSM kupitia maduka na Mawakala wao jijini Dar es salaam

Pia, GSM imeweka hadharani Matawi yake ya mikoani ambayo mashabiki wanaweza kununua jezi za Yanga

ADVERTISE HERE