Uongozi wa klabu ya Yanga umewapokea mashabiki watatu wa timu hiyo waliosafiri kutoka mkoani Mtwara mpaka jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Mashabiki hao waliotumia siku sita kufika Dar, walipokelewa na Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Ruhago

Aidha wote wamekabidhiwa jezi mpya za Yanga na wapata tiketi kwenda kushuhudia mchezo huo
Dk Ruhago amesema kitendo kilichofanywa na mashabiki hao ni cha heshima kubwa kwa Yanga
Amesema ni tukio la kishujaa ambalo linapaswa kuwahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya Jumamosi
ADVERTISE HERE