Pamoja na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United kwenye mchezo wa ligi kuu, mkufunzi wa klabu ya Yanga Charles Mkwasa amesema vijana wake hawakucheza vizuri leo
Akizungumza baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, Mkwasa amesema ratiba ya mechi mfululizo imepelekea vijana wake kutokuwa bora dhidi ya Biashara United
"Tumerejea juzi kutoka Iringa, tumeshinda siku moja tu na leo tumeingia tena uwanjani. Tumetoka kucheza mechi ngumu hivyo nilitarajia mchezo wa leo utakuwa mgumu kwetu kwani wachezaji walikuwa na uchovu," Mkwasa aliwaambia waandhishi wa habari
"Biashara United sio timu mbaya kwani wametupa upinzani mkali. Kama watacheza hivi mechi zote na sio kukamia mechi moja, nadhani watafanya vizuri msimu huu"
"Hata hivyo muhimu tumeweza kupata ushindi na hilo ndilo lililokuwa kusudio letu"
Bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wao mpya Tariq Seif Kiakala aliyeunganisha krosi ya Papi Tshishimbi kwenye dakika ya 85
Ushindi huo umeipandisha Yanga mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 24