Meneja na nahodha wa zamani wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa Januari 04 2020 hautabiriki na yoyote anaweza kufungwa.
Nadir ana uzoefu wa michezo ya dabi kwani amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani miaka 12
Amesema katika mchezo wa watani wa jadi wakati mwingine timu inayoonekana ni bora kuliko nyingine ndio inayopoteza mchezo hivyo ni vigumu kutabiri
"Ni vigumu sana kuitabiri mechi ya Simba na Yanga. Wakati mwingine ile timu inyoonekana kuwa bora zaidi hufungwa, ni ngumu kutabiri," alisema
Tayari tambo kutoka kila upande zinashika kasi kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Januari 04 2020
Wakati Simba ikitamba kuwa na kikosi bora, Yanga nayo haitabiriki hasa baada ya kufanya maboresho ya kikosi chake kuelekea mchezo huo
TFF imewatoa hofu mabingwa hao wa kihistoria kuwa wataruhusiwa kuwatumia wachezaji wao waliowasajili kipindi hiki cha dirisha dogo, muhimu tu wawe wamekamilisha taratibu zote za usajili
Simba haijatangaza kusajili mchezaji yeyote mpaka sasa hivyo ni dhahiri wana imani na kikosi walichonacho