Kikosi cha Yanga jioni ya leo Jumatatu, Disemba 30 2019 kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikaribisha Biashara United ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mchezo huo ni wa kufunga mwaka 2019 ambapo ushindi kwa mabingwa hao wa kihistoria utawapandisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kama Kagera Sugar itashindwa kupata ushindi dhidi ya Ruvu Shooting
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ametangaza viingilio vya mchezo huo kuwa VIP A ni Tsh 15,000/- , VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Akizungumza kuelekea mchezo huo baada ya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Taifa jana, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kikosi chake kiko tayari kupigania alama tatu
Amesema baada ya kufanikiwa kuondoka na alama nne mkoani Mbeya/Iringa, wamejipanga kushinda mchezo huo ili wazidi kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi