Uongozi wa klabu ya Yanga umetaja sababu iliyomfanya kiungo wake Haruna Niyonzima achelewe kuungana na timu licha ya usajili wake kukamilika tangu wiki iliyopita
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kiungo huyo alipewa muda ili akamilishe masuala binafasi na klabu ya AS Kigali
"Mpaka tunaingia mkataba tulikwisha angalia pande zote mbili hivyo Haruna amechelewa kufika kwa sababu alikuwa bado hajakamilisha taratibu nyingine na AS Kigali"
"Tuliona ni busara kumuacha akamilishe taratibu hizo kabla ya kujiunga nasi. Tunatarajia atawasili nchini wakati wowote kuungana na timu," amesema Bumbuli
Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda alitarajiwa kuwasili nchini leo
ADVERTISE HERE