Kule katika mtandao wa Instagram Afisa Habari wa Simba Haji Manara ameshikia 'bango' taarifa zinazodai nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' na beki wa kulia Hassani Ramadhani kuwa walitaka 'kuzichapa' kisa posho.
Hata hivyo taarifa za uhakika na zilizothibitishwa zinabainisha kuwepo kwa tofauti baina ya wachezaji hao baada ya mazoezi jana jioni, lakini hakuna ukweli wowote juu ya sababu ya posho inayovumishwa. Tofauti zao zilikuwa za kawaida tu na zilimalizika baada ya mazungumzo ya muda mfupi.
Ni jambo la kushangaza kwa msemaji wa Simba kuhangaika na mambo binafsi ya Yanga wakati kwake kila mtu anafahamu mambo sio shwari.
Tofauti iliyojitokeza baina ya wachezaji hao sio jambo la ajabu kwani mambo hayo hutokea sehemu yoyote.
Kuna wakati uwanjani wachezaji marafiki wanaweza hata wakakunjana mashati lakini mpira ukiisha urafiki wao unaendelea kama kawaida.

ADVERTISE HERE